Monday, September 10, 2018

Akili ya Eliya Kizazi Cha Nne

AKILI YA ELIYA KIZAZI CHA NNE











Na




















MTUME NA NABII ELIYA AD2 MUNGU WA MAJESHI




UTUME

“Nakutuma ukanijengee Kanisa litakaloniabudu Mimi katika Roho na Kweli.Naliweka Neno langu kinywani mwako, utakaposema nao wakisikia na wakaamini nitawapa haja za mioyo yao (Yn.9:7).
Nimekupaka mafuta ili kuvunja misingi mibaya ndani yao na kuwajenga katika nguzo nne; Neno, Imani, Utii na Utakatifu juu ya Msingi ambao ni Kristo YESU 1Kor.3:10-12

Copyright (c): Mtume na Nabii Eliya Ad2 MUNGU wa Majeshi;
Kimechapishwa nchini Gosheni (Tanzania);
Toleo la 3 Abibu 3, vitabu 5,000; na
Mchapishaji na msambazaji Ni Siloam Ministry International, S.L.P 60486, Dar Es Salaam, Tanzania.
YALIYOMO

Akili ya Eliya ni kituo kikuu kuliko vituo vyote ambavyo kanisa liliwahi kupitia au kufika.Wengi ndani ya Kanisawalikuwa bado na akili za aina mbalimbali kama vile: akili ya Mjerumani; Mwingereza;Mswidishi;Mmarekani;Mrumi; Mwarabu; nakadhalika. Licha ya akili mbalimbali za mataifa yaliyoanzisha dini na madhehebu; kuna akili pia za shule, ukoo, kabila, taifa na mataifa kulingana na ulikowahi kutembelea na kuishi. Hii ndiyo sababu utaona mtu amesoma sana lakini anavaa lubega. Hali ile inaonyesha kuwa mhusika ana akili ya asili ya kabila na ukoo wake. Ukimweleza kitu tofauti na hicho anakujia juu kama mlevi aliyebobea.Katika wiki hii ya limbuko la mwaka wa tatu wa kanisatumefika mahali pazuri pa kupokea akili ya tofauti na akili tulizowahi kuwa nazo .Akili hiyo ya tofauti ni Akili ya Eliya, ambayo hutuwezesha kufungua mlango wa nchi nzuri yenye kila kitu tunachotamani katika ufalme wa MUNGU.
Kama utakavyosoma ndani ya kitabu hiki, utagundua kuwa hadi sasa wote tunahitaji akili moja tu ambayo imemwangamiza kerubi namifumo yake yote aliyopandikiza ndani ya uumbaji wote. Akili hii ni ya Matengenezo, marejesho, upatanisho na kujenga, yaaniAkili ya Eliya(Lk.1:17). Kwa kusoma 1Fal.19:19-21;tunajifunza kwaElisha wa kizazi cha pili kwamba alipokutana na Eliya alihesabu kazi zote alizowahi kufanya zamani kuwa ni manyasiakaachana nazo. Sisi wa kizazi hiki cha nne ni zaidi.
Ufunguo wa kuingia nchi hiyo nzuri ni mtazamo kama huo wa Elisha hatimaye kukiri, hadharani kuwa kila ulichowahi kufanya kabla hujakutana na nabii wa kizazi cha nne ni manyasi.Ili Akili hii ya Eliya ambayo ni akili ya MUNGU mwenyewe iingie ndani yako kwa ajili ya kukuwezesha kupokea vitu vya nchi nzuri ya kizazi cha nne, unalazimika kuliona hilo. 
Akili hii inabariki, ina ushindi, haiogopi chochote, inakuwezesha kuwa na imani juu ya kerubi,inakutoa chini kukupeleka juu kuliko wote, inakuonyesha njia ya watakatifu, imebeba utajiri wote unaohitaji katika ufalme wa MUNGU, nakadhalika.Mtihani ni huo wa kukubali kuwa kabla hujakutana na Eliya wa Kizazi cha nne, hukufanya kazi yoyote ya dhahabu, fedha wala mawe ya thamani. Atakayepata neema ya kuona na kutamka kwa dhati ataingia.
Elisha akifuatana na Eliya kizazi cha pili, walipopita Yeriko walikutana na kikwazo cha mto wa Yordani (2Fal.2:7).Ili wavuke Yordani Eliya alichukua vazi lake la juu akayapigamaji ya Yordani yakagawanyika. Vazi hili la juu ni Akili ya Eliya ambayo Elisha alikuwa amekutana nayo katika 1Fal.19:19 akaamua kuacha kila alichokuwa anafanya na kumfuata Eliya. Walipofika ng’ambo katika 2Fal.2:9penye nchi nzuri, Eliya alimweleza Elisha sasa omba kwangu utakalo nitakupa. Siku zote usisahau, ufunguo wa kuingia nchi nzuri ni Akili ya Eliya. 

1. MWAKA WA TATU WA KANISA NI KUANZA UPYA

Lango la 1 Abibu, 3 MUNGU mwenyewe kupitia Mjumbe wa Mapenzi ya MUNGU alitujengea Madhabahu ya Kufanikiwa na Kubarikiwa Kizazi cha Nne.Madhabahu hii ilijengwa kwa Maombi na Shukrani Maalum kwa kila mmoja aliyekuwa ndani ya Ibada kupita Madhabahuni huku akikanyaga Fedha na Dhahabu.  Neno katika Malaki (Wakati wa Kizazi cha Pili) linasema katika siku hiyo tutakanyaga maadui kama makapi (Mal.4:3).
Kizazi cha Nne, MUNGU alituthibitishia kuwa si tena kukanyaga maadui bali Fedha na Dhahabu kama UKOKA. Kiapo kilitolewa naNabii kuwa ‘Labda MUNGU anikane leo, lakini akinikana, atakuwa amejikana mwenyewe kwa kulikana Neno lake.”

Kwa Kiapo hiki, ni dhahiri kwamba MUNGU hawezi kuacha kulitimiza Neno alilotamka kupitia kinywa cha Nabii Eliya Kizazi cha Nne, kwamba ni lazima sasa tukanyage Fedha na Dhahabu kama Ukoka, kwa sababu ya wingi. Si hivyo tu lango 1 Abibu, 3 Kanisa zima tulipakwa Mafuta ya Akili ya Eliya Kizazi cha Nne ambayo ndiyo Akili ya MUNGU ambayo wengi wameitamani siku zote.

Kabla ya Mafuta hayo ya Akili ya Eliya kila mmoja ajihoji kama ana Mahali pa Akili hiyo kukaa. Hii ni kwa sababu wengi ingawa wameongozwa Sala ya Toba katika Madhabahu Sahihi bado walikuwa na ile hali iliyompata Daudi katika Zab.73:2 ya kuwa karibu na kuteleza.

Wengi walikuwa bado wanafuatisha namna ya dunia hii. Kitu gani husababisha Mwana wa MUNGU aendelee kupenda yaliyoko kule nje? Ni kwa sababu wengi nafsi ya zamani haijafa kabisa.Katika Yn.12:23-24 Neno linasema aipendaye nafsi yake (yaani yale ya zamani tuliyojifunza) ataiangamiza. Bali aichukiaye (yaani yule aliyeamua kugeuka kabisa) ataisalimisha. Neno hili kwa upana wake na urefu wake lina maana hii.

Kuna akili ulipewa na dini au dhehebu au nabii wa uongo uliyewahi kuwa naye ambaye amechora ramani ndani ya nafsi yako jinsi ya kumwabudu MUNGU. Bila kumkana yule aliyekufundisha na kuyakana mafundisho yake, huwezi kupokea Akili ya Matengenezo, Marejesho, Upatanisho hatimaye Kujengwa upya (Akili ya Eliya). Aidha, kuna akili ulipewa na mwalimu wako shuleni kupitia masomo mbali mbali uliyosomea na Ustadi ulionao.

Akili hiyo imetengeneza aina ya tabia na mfumo wa maisha (ambayo hukuwa nayo ulipozaliwa). Bila kumkana yule mwalimu na akili hiyo mbovu au mbaya aliyokupa, Akili ya Matengenezo, Marejesho, Upatanisho, Kujengwa (Akili ya Eliya) haitaingia kamwe.

Kuna akili ulipewa na ukoo uliozaliwa, kabila, lugha, jamaa, taifa na mataifa uliyowahi kwenda kwa kupendelea na kusifia vitu mbalimbali walivyonavyo.

Msimamo huo umeendelea nao kwa sababu ya mizimu ya mababu na mabibi waliokufanyia maagano ya damu na viapo ili kutobadilika. Usipoapa na wewe na kwa kutumia Agano la Damu ya Haki, Kweli na Hukumu, Akili ya Matengenezo, Marejesho, Upatanisho na Kujenga (Lk.1:17) haitaingia ndani yako.

Neno limesema kuwa utabakia vile vile ulivyokuwa zamani na kuanza kulaumu na kulalamika kuwa Nabii hana Mafuta ya kutosha, kumbe ni wewe uliyeng’ang’ania akili ya zamani. Ukiendelea kuwa na akili ya dini, dhehebu, nabii wa uongo, shule, cheo, nafasi katika jamii, Akili ya MUNGU ambayo ndiyo hutupa Nchi Nzuri ya Kizazi cha Nne haitakuingia na UTAACHWA NYUMA.

Unaweza ukaing’ang’ania akili ya zamani, lakini msomaji utakuwa shahidi kuwa waliofuata akili hiyo, sasa wameisha kabisa (Obadia 1:17-18).Ni MUNGU mwenyewe alisema kwamba lazima wote waliodhani wako juu kidunia awashushe (Obadia 1:2-4).Majira hiyo ya wenye akili mbovu kushushwa, imeshafika.
Kwa Nini Tuanze Upya?
Katika Yn.4:23-24 YESU alisema saa inakuja na ipo ambapo wamwabuduo MUNGU halisi watamwabudu katika Roho na Kweli na hao ndio MUNGU aliokuwa anawatafuta siku zote. Aliyepewa Agizo la Kujenga Kanisa Linalomwabudu MUNGU Katika Roho na Kweli na kuvunja Misingi mibaya yote ndani ya watu na mazingira yao ni Eliya Nabii wa Kizazi cha Nne.

Ili afanikishe Agizo hilo amepewaRoho ya Matengenezo, Marejesho, Upatanisho na Kujenga, tumethibitisha hili kwa kipindi cha kuanzia Mwaka 2003 hadi 28 Adari, 2011,Kanisa lilipohamia Rohoni kwa kupokea Majira na Nyakati za Kanisa; sasa ni Kipindi cha Miaka Miwili kamili. Kuna jumla ya Miaka 10 tangu Eliya wa Kizazi cha Nne aitwe.  Katika Kitabu cha Kut.12:29-36 tunakutana napigo la kumi ambalo lilisababisha Farao aachilie Wana wa Israeli kutoka utumwani moja kwa moja ndani ya masaa 12 peke yake.
Kanisa nasi tumefikisha Miaka 10, kutoka ni lazima maana namba kumi (10) humaanisha kutoka.

Wakati wa Kizazi cha Kwanza hata hivyo Wana wa Israeli walitoka pamoja na Wamisri waliochangamana nao (Kut.12:38) ambao walisababisha kulalamika na kunung’unika kule mbele ya safari, jambo ambalo liliwaulia njiani akavuka Joshua na Kalebu peke yao, kwa wale waliotoka utumwani.

Hili ndilo tatizo ambalo halijatokea hata kidogo kwa Israeli ya Rohoni. Agizo limeeleza wazi kuvunja misingi yote mibovu na Mafuta ya kuvunja hiyo misingi yote tumepakwa, lakini bado walio wengi wamevuka na misingi hiyo mibovu ambayo husababisha waendelee kuwa na akili ya: kulalamika, kunung’unika, tabia ya asili, matendo ya mwili, dhambi, uasi na kadhalika. MUNGU wa Eliya ni mwema, ametoa nafasi sasa kwa kila mmoja kujikagua ni wapi alikuwa bado hajatengeneza ili akili mbovu zote alizovuka nazo kutoka Mwaka wa Pili kuingia wa Tatu zifutike iingie Akili ya Eliya ya Matengenezo, Marejesho, Upatanisho na Kujengwa kwa Upya.

Wachungaji

Kama ni Mchungaji, ulianza Kituo, ukapokea Sadaka ya Kwanza ukaila bila kutoa Malimbuko, umevuka na mauti kwako na kituo. Hapo hapo ulipo, Ibada inayofuata Sadaka yake yote hakikisha umetoa Malimbuko ili kuanza upya katika Jina la YESU (Rum.11:16 na Hes.18:12)

Usipofanya hivyo, akili ya Eliya haina pa kukaa katika Kituo chako na ndani yako wewe mwenyewe.

Kama uliwahi kufanya huduma kwenye dini au dhehebu lolote au ukakaa na nabii wa uongo yeyote, fanya zaidi ya Elisha wa Kizazi cha Pili alivyofanya katika (1Fal.19:19-20) kwa kukiri hadharani kuwa, kabla hujakutana na Akili ya Matengenezo, kila huduma uliyofanya ilikuwa ni kuni, manyasi na majani maana ukipitisha kwenye tanuru lazima iungue. Hata kama ulisoma theolojia na kwenda kila mahali, usisite kukiri hadharani kuwa hayo yalikuwa ni manyasi ambayo hayawezi kuhimili moto wa Kizazi cha Nne.
Kubali lile Neno la YESU katika Mt.18:1-4 aliyesema kuwa wote lazima tukubali kuongoka kama vitoto. Mtoto ni mnyenyekevu, anakubali kufundishwa na baba, anatamani kufanya kama baba, anatamani kufanana na baba. Ikiwa hutafanya hivyo umebaki Mwaka wa Pili!

Kama kituo chako kilikuwa hakitoi Fungu la Zaidi ya Kumi, ina maana hata Wana wa MUNGU ulionao hawawezi kutoa zaidi ya Fungu la 10. Wataendelea kutoa Fungu la 10 la Kizazi cha Kwanza hadi cha Tatu, matokeo yake wote mtabaki Mwaka wa Pili!

Ikiwa wewe Mchungaji hutoi Sadaka ya Nabii, hata Wana wa MUNGU hawatatoa, na watakuwa wamekauka, maana ule mto wa Fedha na Dhahabu unakatikia njiani kabla ya kufika Kituoni kwako.

Kama unafundisha Mafundisho yako na si MUNGU alichomwambia Nabii wa Kizazi cha Nne, basi wewe ni LOGOS moja kwa moja na umewaua Wana wa MUNGU (2Kor.3:6). Kwa mantiki hiyo wa kwanza kubadilika Mwaka wa Tatu ni Mchungaji ndipo Mwana wa MUNGU afuate.

Kama Mchungaji ulikuwa unapanda Madhabahuni kufundisha Nenola Siku kutoka kwenye moyo wa MUNGU, lakini ulisikiliza Kanda ya Nabii au kusoma Kitabu chake bila Kujenga Kwanza Madhabahu, hukupeleka Nafsi, Moyo na Roho ya Matengenezo, Marejesho, Upatanisho na Kujenga ndani ya mioyo ya Wana wa MUNGU siku hiyo. Maana hakuna kilichokuunganisha wewe na sauti ya MUNGU ambayo ina adhama (Zab.29:4-5).

Ulitumia akili ya dunia (dini, dhehebu) eti kwa kuwa unajua kusoma Kitabu au kufungua “Music System”uliamka kuendelea tu kama kawaida.

Mwaka huu badilika na ugeuke ili ufanye sawa na Akili ya Eliya Nabii ambayo ni ya MUNGU mwenyewe.

Hata kamahuna fedha ya kujengeaMadhabahu (Fil.4:18)’ bado unawajua wenye shida wainue mbele za MUNGU, na umwambie kuwa hiyo ni Madhabahu umemjengea ili uisikie Sauti ya MUNGU kwa ajili ya Kanisa (Ufu.8:3-5). Siku zote ukumbuke, ukifanya kinyumena Akili ya Eliya Nabii, utashindwa.  Nabii ameshaapa kuwa “HUTASHINDWA KAMWE MILELE.” Huna sababu ya kuendelea na akili ya zamani inayoshindwa. Umeingia Mwaka wa Tatu, Nchi Nzuri Kizazi cha Nne, kubali kupokea Akili ya Eliya ambayo itasababisha ushangaze.

Neno katika Ebr. 6:12 linasema tusiwe wavivu wa kuwa wafuasi wa wale waliorithi Ahadi za MUNGU kwa Uvumilivu na Imani. Wote tumeshuhudia Urithi wa Ufalme wa MUNGU kwa Eliya wa Kizazi cha Nne; kwa Uvumilivu na Imani. Hakuna tena sababu ya kuendelea na akili zilizoshindwa.  Imani iliyomfikisha juu Eliya wa Kizazi cha Nne, na kulifikisha Kanisa juu ni KUTENDA ULICHOAGIZWA NA MUNGU, basi. Hiyo Imani inayokupa kushinda ukiwa katikati ya simba na dubu, wote tunaihitaji. Lakini Imani hiyo haiingii kwa yule mwenye akili ya mila, desturi, asili, matendo ya mwili, sheria ya dhambi,; bali kwa yule mwenye Akili ya Matengenezo, Marejesho na Kujenga (Akili ya Eliya).

Nitajuaje Kama Bado Nina Akili Mbaya?

Ni rahisi kugundua kama bado una akili ya zamani au mbaya, isiyokupa kushinda ili ugeuke.

Kama pale mlima wako wa moto (nyumbani) bado kuna Vitabu vya wanikolai (Ufu.2:2-6) una akili ya zamani ambayo inakataa akili ya Matengenezo, Marejesho, Upatanisho na Kujenga (Akili ya Eliya).

Katika mistari hiyo minne MUNGU anatambua kuwa unachukia matendo mabaya yanayofanywa na wale walioko mwilini. MUNGU anatambua kuwa umekubali Madhabahu sahihi, lakini kwa hilo la kuficha vitabu vya wahubiri wainjili ya Kizazi cha Tatu ili ulinganishe, anasema hapo tu ndipo mlipotofautiana. Ni kwa sababu umeikataa Akili yake ambayo ndiyo ingekuwezesha kuona mwanzo hadi mwisho wa uumbaji. Leo chukua kiberiti na mafuta ya taa uchome vitabu vyote ulivyo navyo vya wanikolai. Kama pale mlima wa moto bado kuna Kanda, DVD na CDs za wanikolai (na wengi wanayo na wanasikiliza) basi wewe akili yako ni ya zamani. Kwa hali hii huwezi kupokea Akili ya Eliya Nabii ambayo ndiyo yenye uwezo wa kukuingiza katika Nchi Nzuri.

Kama bado una moyo wa siri, kufanya baadhi ya mambo ili Mtume au Mchungaji wako asijue, basi bado una akili mbaya ambayo inazuia Akili ya Eliya isiingie. Hili ni kwa Wachungaji na Wana wa MUNGU pia. Chochote ambacho usingependa Mtume na Mchungaji ajue, kimetokana na akili mbaya.

Kama bado unavaa suruali ya kubana, juu unafunika kwa kanga ukiwa kanisani, kisha ukitoka nje ya Kanisa unatoa kanga; basi bado una akili mbaya inayopinga Akili ya Eliya isiingie. Leo ni siku ya kuamua kuwa huru ili upokee Akili ya Matengenezo, Marejesho, Upatanisho na Kujenga.

Mwisho ikiwa bado unasikia kusita kutamka kuwa vyote ulivyofanya kabla ya kukutana na Eliya ni kuni, manyasi na majani; basi ujue WANIKOLAI bado wamejaa ndani yako. Hujawahi kuwakana, kiti cha Akili ya Matengenezo hakitapata nafasi ndani ya moyo wako.Leo nakuhimiza uchague fungu lililo bora.
Kama bado unaogopa kusema Shika-Neno Tenda Nenombele za wanadamu ukiwa labda sokoni, ofisini, kwenye basi au ndege au hotelini; basi ujue wewe una akili nyingi za Kizazi cha Kwanza hadi cha Tatu ambazo zimefeli.Unaogopa kukiri Akili ya MUNGU iliyoshinda.

Kama bado unaogopa kuvaa vazi jeupe mbele za watu na wanadamu. Yaani, jijini una mavazi ya kawaida wakati Vazi Jeupe liko mfukoni ili uje kuvalia Mahali pa Usafi Kanisani; basi Akili ya Eliya haina nafasi kwako. Mwingine, akimaliza Ibada, anavua saa hiyo hiyo na kuhifadhi mfukoni ili akiwa kwenye daladala asijulikane.  Huyo naye Akili ya Eliya haijawa na mahali pake ndani yake. MUNGU akuwezeshe leo kuanza upya.


2. AKILI YA ELIYA NDIYO ILIYOTUINGIZA KATIKA NCHI NZURI

Akili ya Eliya ni Akili ya MUNGU Mwenyewe

Ukisoma katika Isa.40:28-31 ndipo utakapogundua jinsi Akili ya MUNGU ilivyo. Akili hii ya MUNGU ndiyo Akili ya Eliya. Katika 1Fal.17:1 tunapata uthibitisho kuwa Eliya Nabii ana Neno la MUNGUnaana Neno lake pia. Neno la yeyote linatokana na akili yake ilivyo. Kwa mantiki hiyo iliyofunuliwa katika 1Fal.18:21 pia utathibitisha jambo hili kwa sababu ya lile swali alilouliza watu wote kuwa “Mtasita-sita katikati ya mawazo mawili hata lini?”Hii ina maana kuwa nia au hiari ya Eliya ni moja tu!  Mwenye hiari moja katika Kizazi cha Kwanza hadi cha Tatu alikuwa ni MUNGU Baba peke yake.  

Kizazi hiki cha Nne tumepewa Akili ya Eliya ambayo ina Hiari Moja tu!  Kwa mantiki hiyo Akili ya EliyaniAkili ya MUNGU mwenyewe. Uthibitisho kwa hili ni rahisi mno.  Kwa wale ambao wanajua mfumo wa madhehebu ya kilokole ulivyokuwa, kabla ya Kanisa la Mwisho kujengwa, ulikuwa huwezi kukatiza hata mwezi mmoja peke yako bila kwanza kusujudu kwa wazee wa mji (Gate Keepers) ulikuwa huwezi kuendesha Mkutano wowote wa Injili bila wao kutoa ruhusa. Wakisema “hatumtambui huyu”ndivyo ilivyokuwa inatokea.

Kwa kuwa Akili ya Eliya ni Akili ya MUNGU mwenyewe, na haina Hiari ya Pili, baada ya Eliya wa Kizazi cha Nne kupewa Agizo hakwenda kusujudu kwa gate Keeperyeyote kwa kuwa Akili ya MUNGU haimsujudii mtu.
Neno limesema katika Isa. 40:8 kuwa sintachangia utukufu wangu na mtu yeyote. Hata hivyo tukubaliane kuwa bila Akili ya Eliya ambayo ni ya MUNGU, Akili isiyoogopa vitisho, ilikuwa siyo rahisi hata kidogo kulijenga Kanisa likasimama. Atukuzwe MUNGU wa Majeshi kwa ajili ya Akili ya Eliya, ambayo ni ya MUNGU mwenyewe. Haichoki, hairudi nyuma, hainung’uniki, hailalamiki, haihitaji kutiwa moyo na mtu yeyote, haikati tamaa wala kutishika kwa lolote.
Akili ya Eliya Haikai Kwenye Uchafu Wowote

Katika 1Fal.18:17-20 Eliya Nabii alionyesha kuchukizwa na matendo ya Mfalme Ahabu wa Israeli kwa sababu ya kuwafuata mabaali na maashera ambao walikuwa wamezunguka meza ya mkewe.  

Kwa sababu hiyo aliamuru Ahabu na Israeli nzima wamfuate Mlima Karmel ili Eliya avunjevunje kazi na mabaali na maashera, hatimae kujenga upya Madhabahu ya BWANA iliyokuwa imevunjika kwenye Bustani ya Adeni na Edeni (1Fal.18:30).

Katika 1Fal.19:10 Eliya Nabii anatoa taarifa mbele za BWANA kwa sababu ya uchafu ambao Israel walikuwa wameurudisha mahali alipokuwa amekwisha safisha kupitia Madhabahu aliyokuwa amejenga.  Taarifa hii alitoa mbele za MUNGU kwa kuwa Akili ya Eliya haichangamani na uchafu wowote. Aidha, katika 2Fal.1:9-15 tunasoma jinsi ambavyo ukijaribu kushusha chini Akili ya Eliya inavyokushushia moto mkali, uwe mmoja au muwe kundi, akiwa peke yake anawamaliza. Hiki ndicho tunachokithibitisha katika 1Fal.18:40 pia.  Walikuwa jumla ya 850 akiwa peke yake akawafyeka.  Kila anayehitaji utakatifu wa kweli; lazima awe na Akili ya Eliya ambayo haina mjadala na uchafu wa aina yoyote ile.

Akili ya Eliya Haichangamani na Damu na Nyama

Katika Mt.16:16-15 YESU alisema kuwa atalijenga Kanisa lake na milango ya kuzimu haitalishinda kamwe.  Ni mwenye Roho ya Eliya iliyobebwa na Akili ya Eliyapekee anayeweza kujenga Kanisa la Kweli. Hapa hakuna kujifagilia ndivyo ilivyo. YESU mwenyewe, katika Mt.17:10-13 alipoulizwa na wanafunzi wake kuwa “Kwa nini waandishi wote husema kuwa, Eliya lazima aje kwanza?”

Alisema ni kweli lazima aje kwanza ili Kutengeneza yote.  Alipoulizwa tena katika Marko 9:10-11 swali kama hilo na wanafunzi wake alisema kuwa Eliya lazima aje Kurejesha yote.

Majibu haya ya YESU yalikuwa na maana kwamba lile Kanisa alilosema atalijenga na malango ya kuzimu hayatalishinda, ilikuwa ni lazima Akili ya Eliya iingie kazini kwanza kuondoa wezi na wanyang’anyi waliokuwa wamemtangulia YESU (Yn.10:8). Hao ndio waliosababisha YESU apewe Roho Saba za MUNGU (Ufu.5:6) wakati anazaliwa na Mariamu lakini baada ya kazi ya Miaka 33 ½ akaacha Roho moja tu katika (Mdo.1:8) ili wasiendelee kuiba.  Hao wezi na wanyang’anyi ndiyo waliosababisha YESU apelekwe juu ya Kimara cha Hekalu (Mt.4:6-10 naLk.4:5-9) kujaribiwa akakaa kimya. Hii Hati Miliki ya Bustani ya Adeni naEdeni, ambayo kerubi alikuwa amechukua na kuiba kila kitu naniangemnyang’anya bila Akili ya Eliya? Kila mwenye ufahamu akijifunza Njia ya Watakatifu ambayo Kanisa la Mwisho limepitia kutoka chini hadi juu, atakubali kuwa Aili ya Eliya ilikuwa ni ya lazima.

YESU alimweleza Petro katika Mt.16:17 kuwa si damu na nyama vilivyokufunulia hayo bali ni Baba yangu wa Mbinguni. Hapa YESU alikuwa na maana kuwa, mahali Kanisa lilipokuwa linatakiwa kuanzia ni kwenye Chanzo, Msingi na Limbuko la MUNGU mwenyewe (kwenye Kituo cha UFUNUO). Kwa Kanuni na Taratibu ambazo zilikuwepo tangu anguko.  Na kwa jinsi Adam 1 mwenyewe alivyoumbwa wakati tayari kuna mitego ya kumwangusha (na akaanguka), bila Akili ya Eliya, Kanisa lisingevuka.
Akili ya Eliya Haiangalii kama Binadamu Waangaliavyo

Katika 1Sam.16:1-11 tunasoma kuwa MUNGU alimtuma Samwel “Nabii” akampake Mafuta Daudi badala ya Sauli.  Kwa jinsi Daudi alivyokuwa mdogo na anayechunga kondoo, hata baba yake hakudhania kuwa Daudi ndiye angepakwa Mafuta kuwa Mfalme. Walikuja kaka zake na Daudi, baba yake aliamini wana sura za kuwa Wafalme lakini Akili ya MUNGU iliwakataa.  Hata Samweli katika mstari wa Saba, alipomuona Eliabu, mmoja wa kaka zake Daudi, alivyokuwa anapendeza kwa sura, alitaka kuteleza!.  Hapo ndipo MUNGU aliposema na Samweli kuwa yeye ana akili isiyofanya maamuzi kibinadamu, akili hiyo inaona hadi moyoni. MUNGU alisema kuwa wanadamu wanaangalia sura ya nje.

Katika Mwaka wa Pili wa Kanisa, kuna Mchungaji mmoja kati ya Njia Saba za Kanisa ambaye alionekana kuharibu kwa kadri ya ufahamu wa Kizazi cha Kwanza hadi cha Tatu. Ufahamu huu ulisababisha akawa ameondolewa kwenye utumishi moja kwa moja na kurudi alikotokea zamani. Ghafla Akili ya Eliya ambayo ni ya Matengenezo, Marejesho, Upatanisho na Kujenga Upya ikawa imemuona na kurudishiwa utumishi. Matengenezo alipoangalia moyoni kwa Akili ya Eliya, aligundua kuwa aliibiwa utumishi.  Hivyo baada ya Akili ya Eliya kumrejeshea utumishi, anaendelea hadi sasa.  Wote, ili tuangalie kama MUNGU anavyoangalia, tunahitaji Akili ya Eliya.  Kwa Akili hii hakuna atakayepotea wala kufia njiani, kama ilivyotokea kwa wale Wana wa Israeli mwilini.

Akili ya Eliya Inahuisha
Uumbaji wote wa kwanza ulikuwa umejaa mauti. Baada ya MUNGU kumuumba kerubi akiwa mkamilifu (Eze.28:15(a) baadaye akaasi uzima ulipotea.  Ilihitajika Akili ya MUNGU mwenyewe, isiyokata tamaa kuendelea na mpango wa kuumba Mbingu na Nchi (Mwa.1:1).

Hii ni kwa sababu wakati MUNGU anasimama na kusema iwe nuru na ikawepo, tayari giza, ukiwa na utupu walikuwa wanamuangalia kwa pembeni (Mwa.1:2). Ndiyo maana hata Adamu 1 alilazimika kushindwa kutii Agizo alilopewa akiwa katika Bustani ya Edeni (Mwa.2:15-17).Mauti ilikuwa tayari iko pale alipoumbiwa.  Baada ya anguko, ilikuwa mbaya zaidi kwa kuwa hata nafsi hai ambayo ingemsaidia kupambanua lililo jema na lililo baya ilichukuliwa na kerubi, ibilisi, nyoka wa zamani.

Tunaona katika Eze.28:1-10 kerubi akijiita mungu, akitamba kuwa ana moyo wa MUNGU na kwamba hafichwi kitu chochote kile kwa sababu hiyo aliteka nyara kila alichowahi kuumba MUNGU kwa miaka yote, kwa Vizazi vyote.  Kila aliyeinuka akiwa ametumwa na MUNGU alimuua (Mt.21:33-39).

Kerubi aliua kila kitu na akatutenga kabisa na MUNGU.  Hapakuwepo tena na matumaini ya watu na wanadamu kupokea Wokovu wa Kweli. Wachungaji na Watumishi wa wa aina mbalimbali ambao walijaribu kuinuka wakipewa fedha kidogo tu walikuwa wanaasi.  Mwingine akipata gari zuri tu alikuwa anaishia hapo hapo. Wengine walizinina washirika wao. Tena hao ndio wengi, wakafa kiroho moja kwa moja hata kama tunawaona wanatembea barabarani.! Waliojiita makanisa ya kiroho ndiyo usisema, walidharauliwa kupitiliza wakasababisha MUNGU atukanwe! Hawakujua wafanye nini. Wengine walienda porini kufunga na kuomba, wakafia huko.

Akili ya Eliya ndiyo imetufanya Adamu wa Pili ambaye ni Roho inayohuisha.

Katika 1Kor.15:43-45 Neno linasema kuwa Adamuwa Mwisho ni Roho inayohuisha.  Kwa nini Adamu wa Pili au wa Mwisho ni Roho inayohuisha?
Kuanzia mstari wa 43, Neno limefafanua kuwa ulipozaliwa na baba na mama ulipandwa katika uharibifu, lakini kwa sababu ya kukutana na Nabii mwenye Akili ya Matengenezo, Marejesho, Upatanisho na Kujenga umefufuliwa katika fahari. Hii ni kweli kwa sababu waliokuja na ukimwi na kansa au saratani za aina mbali mbali wameshuhudia kupokea uponyaji. Magonjwa yote ni mauti lakini ukimwi au saratani ni Zaidi. Shuhuda zipo nyingi za walioponywa ukimwi na saratani na magonjwa mengine mengi, kwa maana ya kuhuishwa wakati walikuwa wanahesabiwa kufa. Ulipozaliwa na baba na mama ulipandwa katika mwili wa asili. Lakini baada ya kukutana na nabii mwenye Akili ya Matengenezo, Marejesho, Upatanisho na Kujenga umefufuliwa katika roho. Mmoja wa wana wa MUNGU ambaye anafanya kazi nchini Libya alipimwa damu na kampuni yake kwa kutumia vipimo vya mashine za aina mbalimbali ikaonekana kuwa hana damu kwa group zile ambazo tumezoea za A, B, O na kadhalika. Wale wataalamu ambao walimpima walishituka kuwa huyu ni mtu au mwanadamu wa aina gani ambaye damu yake haijulikani ni group gani. Mwanzoni yeye alishituka kuwa labda wamekuta ana ukimwi, hasa kabla hajaitwa kuulizwa. Ndipo alipopiga simu kwa Nabii Eliya na kumweleza jinsi ambavyo ukiokoka kwenye madhabahu ya kweli, neno linasema katika Yn.1:12-13 kuwa huzaliwi tena kwa mapenzi ya mtu wala mwanadamu bali mapenzi ya MUNGU mwenyewe. Hilo likampa nguvu ya kwenda kufuatilia majibu ya damu aliyopimwa na kujikuta akiulizwa maswali mazito. “Wewe unatoka wapi na ni kabila gani ambaye damu yake haijulikani? Ukimwi huna wala ugonjwa wa aina yeyote, lakini damu yako haisomeki kwenye mashine za sayansi!”Ndipo yule mtumishi alipoamini neno la nabii kuwa kweli Akili ya Eliya inahuisha. Alipandwa na baba na mama katika mwili wa asili lakini sasa amehuishwa katika Roho. Haya si kila mmoja anayeitwa mtumishi wa MUNGU bali ni yule tu mwenye Akili ya Eliya. 
Hivyo Akili ya Eliya inahuisha, inafungua, inabariki, inatofautisha, haishindwi kabisa. Bila Akili ya Eliya tusingeweza hata kidogo kufikia kiwango cha kuwa Adamu wa pili. Ilihitajika Akili ya MUNGU mwenyewe kutuelekeza jinsi ya kutoka kwenye asili na kuingia katika uungu, kama neno linavyofunua katika Kol.1;13.
Akili ya Eliya ina Mwanzo na Mwisho

Wote tuliokulia kwenye dini na madhehebu na hata waliosoma theolojia, walifundishwa kuwa wa kwanza kuumbwa ni Adamu na Hawa, kama tusomavyo katika Mwa.2:7 na Mwa.1:26-27.Hakuna aliyeona sawa sawa kilichokuwa kimeandikwa katika Eze. 28:13-15 kuwa aliyeumbwa wa kwanza ni kerubi! Aidha hakuna aliyekuwa amefuatilia Ufu.12:1-3 ambayo inaonyesha wazi nafasi ya Kanisa na nafasi ya kerubi kabla na baada ya kuumbwa.  Suala la Adamu 1 kuwa wa kwanza kuumbwa na kwamba dhambi ilianzia pale Bustani ya Edeni, limefundishwa na Vitabu vingi vimeandikwa lakini haikuwa sahihi.
Baada ya Akili ya Eliya, ambayo tulitangulia kuona kuwa ni ya MUNGU mwenyewe, ndipo tumegundua na kuelewa kuwa kabla ya Adamu na Hawa yalikuwepo maisha na kizazi cha kerubi kilikuwepo.Ukifunuliwa sawasawa kupitia Eze.28:13-18(b)utaona kuwa:Neno lilikuwepo pale kwenye Bustani ya MUNGU;Imani ilikuwepo; Utakatifu ulikuwepo pale naUtii ulikuwepo pia kabla ya uasi wa kerubi.
Aidha utumishi nao ulikuwepo kabla ya Adamu na Hawa.

Ufu.12:1 inaonyesha kuwa MUNGU alikusudia kuweka kila kitu chini ya miguu ya Kanisa (mwanamke mwenye Taji na Nyota Kumi na Mbili kichwani huku mwezi ukiwa chini ya miguu yake).Huu ndio mwanzo sahihi ambao umefunuliwa na Akili ya Eliya. Kanisa hapo lazima lijue kuwa hawa waliokuja (ishara ya pili) baada ya Kanisa kuonekana ndani ya Moyo wa MUNGU (Ufu.12:3)hawatakiwi kutusumbua. Tungejuaje bila Akili ya Eliya?

Mwisho naye alikuwa hajulikani vizuri.  Tukisoma katika Ufu.1:10 Yohana anatueleza jinsi alivyokuwa katika Roho Siku ya BWANA, yaani Siku ya Saba (ikiwa na maana ya ile miaka 1,000 ya kutawala na Kristo katika Ufu.20:4-6). Wengi wakisoma katika Mt.24:36 kuhusu siku ile na saa ile, walikuwa wanachanganyikiwa bila kujua kuwa ni ile miaka 1,000 ya kutawala na Kristo. Aidha, hakuna aliyekuwa amejuakuwa: siku ile, siku hiyo, siku ya mwisho; miaka 1,000 ya kutawala na Kristo, siku ya saba; siku ya BWANA; Sabato; zote hizo ni kitu kimoja kumaanisha Siku ya Mwisho!

Ni kweli Akili ya Eliya ina Mwanzo na Mwisho wa Uumbaji wote. Katika 1Kor.15:20-26 Neno la MUNGU limeweka wazi kuwa Mwisho ni lazima arudishe kwa MUNGU Baba Ufalme wake; utawala wote wa uumbaji; mamlaka na nguvu.  Hii ina maana bila Akili ya Eliya yenye Mwanzo na Mwisho, yaliyoibiwa na wezi na wanyang’anyi ndani ya Kanisa yasingerudishwa. Yangeendelea kutumiwa na waovu kulipinga Kanisa wakati huu wa siku ya Bwana.  Ukikosa Mwanzo safari haipo, na ukikosa mwisho, hata kama ulikuwa ulishaanza safari hufiki. Unahitaji Akili ya Eliya yenye Mwanzo na Mwisho.

Akili ya Eliya ina Imani Nyingine Juu ya kerubi

Kanisa la Mwisho lina Agano la kuwa juu ya Yote, Vyote na Wote.  Jambo hili linamaanisha kitu gani? Ukisoma katika Eze.28:1-10 utafunuliwa kuwa kerubi baada ya kumwibia Adamu nafsi hai, alifanikiwa kurudi pale alipoumbwa na MUNGU akiwa mkamilifu.

Neno linatuonyesha kuwa, hakurudi na sura ya kerubi tena bali ya Adamu. Alikalia kiti cha Adamu, ambaye katika Mwa.2:19 tunafunuliwa kuwa alishirikiana na MUNGU katika uumbaji wa ndege na wanyama.  Ukichanganya zile kazi alizokuwa anafanya kabla ya kuasi (ambazo zilikuwepo bado) na uungu alioiba kwa Adamu alitamba mbele za MUNGU (Ayu.1:6) kwa miaka mingi hadi Akili ya Eliya ilipomshusha pale na kumfungia gerezani milele.

Msomaji utakuwa umewahi kusikia dini wakisema habari za mahali pema peponi. Hapo ndipo kerubi alipokuwa na uungu alioiba kwa Adamu. Alikuwa anawapeleka pale wale wote wanao mtii. Akili iliyomtoa pale ni ile ambayo iko juu yake. Mwana wa MUNGU unaposema kuwa kwa Agano la Kuwa Juu ya Yote, Vyote na Wote, lazima uwe juu ya hapo alipokuwa kerubi na waovu wenzake. Bila kuwa hapo huwezi kutiisha uumbaji. Hivyo ninavyoandika kuwa Akili ya Eliya ina Imani nyingine juu ya kerubi, ina maana ni Imani ambayo inakupa kuishi Rohoni juu ya mahali kerubi alipowahi kufika.
Hapo mahali pema peponi, kabla ya kubomolewa na Akili ya Eliya, ndipo waovu walikuwa wanatengenezea magonjwa ya mlipuko, majanga mbali mbali katika jamii, umasikini na kila aina ya shida. Kila aina ya uchafu uliokuwa unaendesha ulimwengu na dunia ulikuwa unatengenezewa hapo. Taratibu na Kanuni mbalimbali pamoja na taasisi kubwa za dunia kabla ya Akili ya Eliya kutamalaki, zilikuwa zinaundwa hapo.

Tunamshukuru MUNGUaliyetupa Akili ya kutenda kile tu ulichoagizwa na MUNGU. Hiyo ndiyo Imani ya Akili ya Eliya ambayo imeliweka Kanisa juu ya kerubi na wafuasi wake wote, katika Jina la YESU.

Akili ya Eliya Inafunua Mambo ya Siri na kuyaweka wazi

Habari ya Miezi ya Kiungu ambayo iko ndani ya Kitabu cha Neno la MUNGU, Miezi ya Abibu hadi Adari (Esta 3:7) Si kwamba wasomi watheolojia, falsafa na saikolojiawalikuwa hawaijui.  Tatizo ni viapo na maagano waliyokuwa wameingia vya kutofunua Siri hii ya Mafanikio kwa Kanisa.

Hata kweli kuhusu Kitabu cha Neno la MUNGU walikuwa wanaijua (Mdo.19:23-34) maagano ambayo yalifanyikia mahali pema peponi (ambapo ulikuwa ni Mlima wa BWANA) kabla ya uasi wa kerubi, ndiyo yaliyokuwa yanawazuia kutamka hadharani.  Bila Akili ya Eliya ambayo iko juu ya akili ya kerubi ilikuwa haiwezekani hata kidogo kupenya! Habari ya wizi wa nguvu za Rohoni Kizazi cha Kwanza  hadi cha Tatu ambazo zilikuwa zinatumika kwa ajili ya kupinga Kanisa la Kweli, imewekwa wazi na Akili ya Eliya.
Akili ya Eliya Imebeba Kazi za Dhahabu, Fedha na Mawe ya Thamani

Katika Kitabu cha Dan. 2:29-35 Neno linaonyesha wazi hasa katika  mstari wa 34 na 35, kuwa sanamu ya Nebkadreza ilisambaratishwa na jiwe ambalo halikuchongwa na mikono ya mtu wala mwanadamu. Katika 1Pet. 2:5-8 Neno linaonyesha kuwa Kanisa ni jiwe wakati YESU ni Jiwe Kuu la Pembeni, ambalo waashi walikuwa wamelikataa mwanzoni.

Sanamu ya Nebkadreza inawakilisha muunganiko wa Wakaldayo au Waajemi, Wayunani, Warumi na dini ya Kirumi.  Muunganiko huu kwa akili ya kibinadamu ulikuwa hauwezi kuvunjika hata kidogo.  Ndiyo maana MUNGU mwenyewe imebidi, ashuke kama anavyosema katika Mt.21:40-41.

MUNGU ni Roho nao wamwabuduo inawapasa wamwabudu katika Roho na Kweli. Kizazi hiki cha Nne, Kumwabudu MUNGU ina maana ya Kutenda kile alichosema, siyo kuinua mikono juu na kuanza kuimba kwa mwendo wa polepole.
Akili hii ya Kutenda tu ulichoagizwa na MUNGU na si zaidi hiyo ndiyo Akili ya Eliya.


Waliokuwa wamebeba kazi  za Dhahabu, Fedha na Mawe ya Thamani kabla ya Akili ya Eliya ni hao waliotajwa kwenye hiyo sanamu.  Bila Akili ya Eliya, hakuna ambaye angewagusa katika ulimwengu wa roho chafu.  Kulikuwa na maagano ya kutisha ambayo yaliziba kabisa ili Kanisa lisije likatokeza tena.  

Maaganonaviapo vyaKanisa kupitia Akili ya Eliyandiyo yamevunja vunja viapande vipande hiyo sanamu ambayo madhehebu yote kwa kufunga na kuomba walishindwa.

Akili ya Eliya Inathubutu Kutenda Ulichoagizwa na MUNGU

Katika Mwaka wa Tatu wa Kanisa, tumeingia katika Nchi Nzuri. Kilichotuingiza katika hiyo Nchi Nzuri ni Akili ya Eliya ambayo imebeba kuthubutu kufanya kile ambacho unatamani hata kama mazingira kwenye uumbaji uliofunuliwa hayaonekani kuruhusu jambo hilo.

Nitatoa shuhuda kadhaa kulithibitisha jambo hili.Wakati tumejenga Kanisa la Mlima wa Maono ya MUNGU,katika muonekano uliopo sasa.  MUNGU aliongea namiasubuhi nianze kuvunja Ofisi yangu mwenyewe wakati hapakuwa na fedha kwenye Hazina ya Kanisa.


Fedha ya kuanzia iliyokuwa inatakiwa ni kiasi cha Hazina 50 (Milioni Hamsini).  Nilikuwa nimesikia sauti peke yangu nikiwa karibu na pale mlango mkuu wa Magharibi.  Baada ya kuisikia sauti, niliamuru saa ile ile Ofisi yangu ivunjwe.  Ilikuwa ni Siku ya Ibada ya Marejesho wakati huo, zikiwa zimebakia siku tatu ili ifike Siku ya Ibada Kuu. Nilipo waarifu Wana wa MUNGU Siku ya Ibada, tena mwishoni alichosema MUNGU, zilipatikana saa hiyo hiyo Hazina Hamsini na Nne (TShs.54, 000,000/=).

Kuanzia hapo gorofa 3 urefu wa mita 30 na upana wa mita 8 zilikamika ndani ya siku 150 peke yake.  Hiyo ni kutokana na Akili ya Eliya ambayo inakupa kutoogopa kufanya kile alichoagiza MUNGU. Huhitaji kufanya majadiliano na yeyote kama MUNGU ameshasema, wewe ni kufanya tu.

Kule Mlima wa Neema Kubwa tulikuwa na Jengo ambalo limekaa karibu Mwaka Mzima bila kuezekwa.  Nilipoenda pale nilikuta hakuna fedha kabisa. Fedha zilizokuwa zinahitajika ni kiasi cha Hazina Sitini (Tshs.60,000,000/=) kwa ajili ya vyuma vya kenchi na Hazina Kumi na Nane (TShs.18,000,000/=) za kununua mabati. Hapakuwepo na chochote wakati MUNGU aliposema kuwa tuanze kazi.  Niliwaeleza Wana wa MUNGU pale wakatoa kiasi cha Hazina Saba (TShs.7,000,000/=).
Baada ya kuwaeleza kuwa haitoshi, Wana wa MUNGU watatuwalitoa viwanja kila mmoja.  Tulipoviombea kiwanja kimoja kilinunuliwa Hazina Arobaini (Tshs.40,000,000/=) fedha ikawa karibu na kiasi kinachotakiwa kupata kenchi.  Ninavyoandika ushuhuda huu, Kanisa tayari limeezekwa.

Kule Toba ya Kweli (Mbezi Luis)ili kuwa vivyo hivyo.  Siku nimeagizwa na MUNGU kwenda kuanza ujenzi nilikuta kuna Laki Saba (TShs.700,000/=).   Fedha iliyokuwa inatakiwa  jioni ilikuwa zaidi ya Hazina Tatu ili kazi ifanyike kama MUNGU alivyo kusudia.  Nilipoagiza kama MUNGU alivyosema kuanza ujenzi mara moja, fedha kiasi cha Hazina Tatu na Nusu (TShs.3,500,00/=)zilipatikana siku hiyo hiyo.
Hivyo Akili ya Eliya imebeba kuthubutu kufanya kile ulichoagizwa hata kama unaona mazingira hayakubali.

Usipokuwa na nguvu ya kuthubutu iliyoko kwenye Akili ya Eliya, huwezi kuingia katika Nchi Nzuri iliyoko ndani ya ufahamu wako wewe mwenyewe (Kumb.8:1-16).

Akili ya Eliya ina Uambukizo na Inatambulisha Mwana wa MUNGU

Hili halikuhitaji maelezo mengi sana.  Linathibitika kupitia watumishi wote walioko kwenye Vituo mbali mbali kwenye Madhabahu ya Kanisa la Mwisho.  Kupitia Agizo alilopewa Nabii wa Kizazi cha Nne, Madhabahu ya Kanisa imejengwa. 
Huduma zote zinafanyikia juu ya Madhabahu ya Kanisa yenye Hekima ya MUNGU katika Siri (Efe.3:10).  Agizo hili ambalo ndilo limejenga Madhabahu ya Kanisa na linalothibitisha kila Huduma inayofanyika juu ya Madhabahu, limetupa Roho ya Huduma. Hiki ndicho kiini cha uambukizo kutoka kwaMbeba Agizo/Maonohadi kwa kila mmoja aliyefunuliwa kwa Akili ya Eliya.

Mama mmoja katika Mwezi wa Adari, 2 alikuwa nyumbani anapika mikate akakutanishwa na mgonjwa aliyekuwa amekaa hospitalini kwa wiki mbili.  Mgonjwa huyu alianza kwa kujikuna kidogo, matokeo yake kuanzia magotini hadi kwenye unyayo akawa kama vile ameungua ngozi.  Mama huyu hana hata muda mrefu akiwa ameokoka.  Kwa kutambua kuwa Akili ya Eliya imebeba uambukizo, alikamata miguu ile iliyokuwa imeungua na kutamka “Hii mikono siyo yangu, bali ni ya Eliya anayeomba siyo mimi bali ni Eliya”  Alipomaliza alimpatia yule mgonjwa Damu ya Haki, Kweli na Hukumu.  Baada ya siku tatu alipigiwa simu ya ushuhuda kuwa aliyekuwa mgonjwa amepona kabisa.

Hii inatokana na uambukizo uliobebwa na Akili ya Eliya. Kwa mantiki hii hii, Akili ya Eliya ina kitambulisho kwa kila aliyefunuliwa rohoni. 
Ukishapata uambukizo, utatofautishwa.  Ukitofautishwa, kila aliyekujua zamani atakuona una jambo la ziada kwa ajili ya utukufu wa MUNGU (1Fal.18:36-39).
Akili ya Eliya Ina Njia ya Watakatifu

Tangu siku ya kwanza nilipoanza huduma, nilianza kufundisha kuvunja madhabahu mbovu za shetani na uzao wake na kumjengea BWANA madhabahu popote uendapo kufanya huduma ili ufanikiwe.   Hii ni kwa sababu MUNGU alinieleza tangu siku ya kwanza aliponiita kuwa mimi ni nani, ingawa sikusema mwanzoni kwa kuwa wengi wangeogopa na kushindwa kufuatilia mafundisho.  

Jambo la pili, nilitangaza tangu mwanzo kuwa nina:

(i) Hiari moja tu, ambayo ni (1Fal.18:21)  na;
(ii) Nina neema kubwa kuliko yeyote ndani ya uumbaji.  
 
Jambo hili liliwashangaza wengi kwa kuwa ukiniangalia kwenye uumbaji uliofunuliwa ulikuwa huwezi kuyaona hao. 
Yote hayo ni sifa kuu za Eliya, hata kama pale mwanzoni sikujitaja kwa jina.  Nakumbuka lango la 16 na 17 Buli 2007 nilipojenga madhabahu ya Kanisa kwa upya, waliokuwepo, hasa wale wenye ufahamu wa dini a madhehebu walishangaa kuwa huyo ni nani ambaye anaweza kujenga hii madhabahu. 
Hata hivyo baada ya pale, hasa wale waliokuwa na mwanga kiasi kuhusu Kanisa linavyotakiwa kuwa walishangaa na kuona kuna jambo jipya.  Hapo ndipo, nilipotangaza rasmi kuwa anayeenda kuhiji Israeli ya mashariki ya kati hana ufahamu kuwa MUNGU  amekwishahama kule Israeli ya mwilini na sasa yuko katika Israeli ya Rohoni, ambayo ni kanisa la kweli.Nilirejesha mambo sita yaliyokuwa yameibiwa katika Rum. 9:4na hatimaye tukapokea, mwaka uliofuata MUNGU kutufunulia majira mpya, kupitia madhabahu hiyo ya Kanisa. 

Ni kitu gani kilichoniwezesha kurejesha hiyo madhabahu ya Kanisa au ya Israeli, wakati neno katika 1Fal.19:10-14 linasema ilivunjika?  Ni Roho ya Eliya ambayo ina kutengeneza, kurejesha, kupatanisha na kujenga.  Bila Roho hiyo huwezi kutamka jambo lililopotea kizazi cha pili likarudi tena kizazi hiki cha nne.  Kwa hiyo ninamshukuru MUNGU  kwa ajili ya madhabahu ya Eliya, ambayo ikiwa mahali popote, nyingine zote zinanyamaza kimya.  Aidha, namshukuru MUNGU kwa ajili ya madhabahu ya Eliya kwa kuwa imerejesha madhabahu ya Kanisa ambayo ni Israeli ya rohoni, iliyokuwa imeibiwa uana, maagano, utukufu, neno, ahadi na ibada katika Roho na kweli (Rum.9:4).  Bila madhabahu hii ya Kanisa kurejeshwa Kanisa lingeendelea kulia tu na kuomboleza bila kujibiwa kwa kuwa lilikuwa halina mahali pa kukutania na MUNGU.
Yumkini, mwingine bado anajiuliza kuwa madhabahu hii ya Eliya imejengwaje na aliyezaliwa mwilini kule Kilimanjaro?  Ukisoma vizuri katika Lk.1:8-17 utagundua kuwa wakati wa kizazi cha tatu Zakaria kuhani na Elizabethi walimzaa Yohana mbatizaji, ambaye alizaliwa akiwa na Roho ya Eliya ya matengenezo, marejesho, upatanisho na kujenga.  Hivyo siyo ajabu mzee Hekima ya MUNGU ambaye zamani aliitwa Zebedayo na mama Neema Kubwa kumzaa mwana mwenye roho ya Eliya, katika kizazi hiki cha nne. Katika hili naendelea kumtukuza MUNGU kwa kulitendea kanisa maajabu!
Katika Mt.21:33-43, hasa mstari wa 40 na 41 MUNGU  anaonyesha wazi kushuka mwenyewe ili kuhukumu wabaya wote. Hii ni madhabahu ya MUNGU mwenyewe ambayo imedhihirika kupitia madhabahu ya Eliya. MUNGU asingeweza kushuka kama alivyo bila kupitia katika hekalu alilolichagua la mjumbe wake kama anavyosema katika Mal.3:1-5, katika hili nampa MUNGU shukrani zangu zote.
Njia Hiyo kwa Ufupi
Kulingana na mambo yalivyokuwa yamefungamana, kama huna MUNGU ndani yako ilikuwa ni vigumu kujua uanzie wapi, upite wapi na uishie wapi! Lakini kwa kuwa MUNGU alikuwa nami, na alinipa Agizo Yeye Mwenyewe, alinielekeza nianze kwa kuvunja misingi mibaya ndani ya kila aliyekuwa anakuja Kanisani. Na alinifundisha Yeye Mwenyewe jinsi misingi mibaya inavyokaa kwenye nafsi za watu. Wakati huo, wanaoitwa makanisa ya kiroho, waliokuwa wamenizunguka, walianza kupiga kelele sana kuhusu mafundisho ya utendaji wa nafsi na kuvunja madhabahu ndani yake. Kazi hiyo kama ilivyokuwa kwa Mtume Paulo katika Gal.1:15-18, niliifanya kwa miaka mitatu mfululizo ili niweze kuzaa watumishi wengine wa kunisaidia kuanzisha Vituo vingine vinavyofanana na mahali nilipoanzia. 

Katika kipindi hicho cha Mwaka 2003 hadi 2006, niliweza kuzaa Vituo vya Elimu (Arusha); Miaka Nane (Boma Hai–Kilimanjaro); Galilaya (Makambako); Marejesho (Kibaigwa–Dodoma); Mlima wa Neema (Morogoro). Shilo Nazaidi (Songea) na Patmo Ufunuo (Iringa). Wote niliowatuma kule walikuwa tayari wanajua mahali pa kuanzia, yaani kuvunja kwanza misingi mibaya ndani ya watu na maeneo yao ili wawajenge juu ya msingi wa Kristo YESU kwa upya (1Kor.3:10-12).

Baada ya Vituo hivyo, namshukuru MUNGU kwa kuwa sasa hivi Kanisa lina Vituo Nchi nzima na tumeshaanza katika Mataifa ya jirani.

Baada ya kuvunja misingi mibaya na kuona tulivyofanikiwa, mwaka 2007, MUNGU aliniambia “Sasa nijengee Madhabahu ya Kanisa kwa upya, kama nilivyotangulia kusema kule nyuma kwa kuwa nafsi za wale wanaokuja ibadani zilikuwa zimeanza kukaa vizuri; MUNGU alitaka atamalaki ndani yao. Nilirejesha kwa Neema ya BWANA, hiyo Madhabahu ya Israel iliyokuwa imevunjwa; kama Neno lisemavyo katika 1Fal.19:10-14. Baada ya hapo, kazi ilianza kuwa nyepesi maana yote yaliyo andikwa katika Rum.9:4 yalianza kutimia:
+Wana wa MUNGU;
+Utukufu wa MUNGU;
+Maagano kati ya Kanisa na MUNGU;
+Neno la Kweli;
+Ahadi za MUNGU kutimia;
+Ibada katika Roho na Kweli.
Huu ndio mwaka nilioandika kitabu cha kwanza kinachoitwa “Faida ya Kumwabudu MUNGU katika Roho na Kweli”

Mwaka uliofuata wa2008 kama nitakavyofafanua baadaye MUNGU alisema nami kuwa bado niko katika Majira na Nyakati za dunia na ulimwengu, hivyo nililitoa Kanisa huko. 

Hapo ndipo aliponionyesha Miezi 12 ya Kiungu yaani:Abibu hadi Adari (Esta 3:7); Siku 7 za Kiungu katika Kitabu cha Mwanzo 1 yote naMwa.2:1-4. Alinieleza pia jinsi ambavyo Vizazi vyote vilivyokuwa vimepita jinsi walivyokuwa kwenye Majira ya Miaka 6000 ya dunia na ulimwengu na jinsi ambavyo inanipasa nirejeshe ile Miaka 1000 katika Ufu.20:4-5. Tunamtukuza MUNGU kuwa, tangu kipindi hicho hasa Mwaka wa 2009 hatukuendelea tena kusherehekea wanachoita Krismasi ya tarehe 25 Desemba kila mwaka wala kusherehekea Pasaka ya duniani ya kila Mwezi Aprili.Tulifanya hivyo kiunabii kwaMiaka 3½ na hatimae ilipofika 28 Adari, 2011tukahamia Majira Mpya ya Kanisa, moja kwa moja kiufahamu. Yote yaliyorejeshwa, Kanisa lote na MUNGU wetu, tunaishi pamoja katika majira na nyakati mpya.
Katika mwaka uliofuata wa2009, MUNGU alisema nami tena kupitia Isa.65:17 kuwa amefanya jambo jipya kwa maana ya Mbingu Mpya na Nchi Mpya.  Huu ulikuwa ni utendaji mpya lakini pia ni kuvunja misingi mibaya ya maeneo tunamoishi.  Kila mahali utakuta kuna maagano ya damu yaliyofanyika ambayo yalikuwa yanazuia MUNGU kupita ili atengeneze.

Hivyo ilibidi kila mahali Kanisa au Kituo kinapoanza kupaita jina jipya la Kiungu ili wachawi, washirikina, wanga na wasoma dua mbaya washindwe moja kwa moja kuwadhuru Wana wa MUNGU.

Lakini pia ilikuwa ni kuwafungua watu wote na Taifa pia ili zile mali kama vile madini na utajiri wa asili, ambao MUNGU aliweka mahali uweze kuwafaidia wanoishi hapo, kinyume na ilivyokuwa mwanzoni, kwamba mpaka ukawatambikie. Tunamshukuru MUNGU kwa kuwa hili nalo MUNGU ametufanikisha tunapata shuhuda nyingi.

Nikupe ushuhuda wa Mbingu Mpya na Nchi Mpya ili uelewe ina maana gani. Mmoja wa wachungaji wangu, alihudumia familia iliyokuwa imetokea Uingereza. Walienda Zanzibar, wakati wanarudi Dar es Salaam, Boti ikazima injini zote mbili. Boti lilianza kupepesuka kuelekea Visiwa vya Comoro kwa upepo mkali sana. Ndipo, kwa ufahamu wao wakaona wampigie mchungaji wao simu kumuaga ili asiwatafute (yaani ajue walikofia). Kila mmoja ndani ya Boti alianza kulia na kuomboleza. Walipompigia na kumweleza kilichowapata, ndipo akawaeleza hivi kuwa “Hiyo Boti mliyopanda ni gari la Eliya la moto; hiyo bahari nayo siyo ya Hindi, bali ni bahari ya Damu ya YESU, na huko mnakokwenda siyo Dar es Salaam bali ni Jiji la Siloam” Aliwatoa kwenye mbingu na nchi zilizofanyiwa mitego ya kichawi, akawaingiza kwenye Mbingu Mpya na Nchi Mpya, sawa na Isa.65:17.

Alipoamuru injini za Boti ziwake kwa Jina la YESU, kupitia simu, injini ya kwanza iliwaka na kisha ya pili, na upepo ukatulia na kila mmoja kule ndani akashangaa na kuanza kuuliza walikuwa wanaongea na nani?  Boti ikarudi kwenye mwelekeo wake wa mwanzo na safari ikaendelea. Waliposhuka kutoka kwenye Boti pale Bandarini, wote walienda kumwona huyo Mchungaji wangu aliyeko Mti wa Neema (Bunju). Hicho ndicho MUNGU alichonipa, huo Mwaka wa 2009.
Katika Mwaka wa 2010, ilikuwa imetimia Miaka 7 ya Kanisa ambayo kwa mujibu wa Kumb.15:1-6 nilitangaza maachilio. Maachilio haya yana maana ya mafundisho ya Madhabahu ya utajiri, ili kila mmoja ndani ya Kanisa apate kuona faida ya Wokovu wa Kweli. Aidha ni kipindi ambacho mimi mwenyewe nilianza kupata nafasi ya kutembelea Vituo vya Mikoani ili kuwajengea Madhabahu ya kumiliki na kutawala mazingira yaliyowazunguka, ikiwa na maana ya uwezo wa kutumia rasilimali walizo nazo, bila kutegemea misaada ya nje. Ninamshukuru MUNGU sana kwa kila Mwana wa MUNGU amelitambua hilo kuwa utajiri hauji kwa kupokea misaada bali kwa kuanzia shambani kulima mazao na kufuga na kushughulika na kazi yoyote unayoiweza ili usiwe tegemezi. Nilianza kufundisha kujiajiri na wengi wanatoa shuhuda Kanisani za kuanzisha Viwanda vyao wenyewe. Namtukuza sana MUNGU kwa ajili ya jambo hilo.

Katika mwaka uliofuata wa2011, Lango la Neema lilifunguka ambalo ukiwa nalo, huzuiliwi chochote. Hili ndilo Lango lililomleta YESU kipindi kile alichozaliwa na Mariamu kama tunavyosoma katika Lk.1:26-30.

Huyu Mariamu alikuwa hajaokoka na alikuwa mwilini, lakini kwa sababu ya Chumba cha Neema alichokuja nacho YESU, hakuguswa na uovu wowote wa Mariamu, kwa maana ya hiari ya pili iliyokuwa ndani ya kila aliyezaliwa baada ya Mwa.5:3. Hili lango ndilo lilituwezesha hatimaye kufikia Majira na Nyakati Mpya za Kanisa mwishoni mwa huo mwaka. Safari hiyo imewezekana kwa sababu ya kutembea na MUNGU bega kwa bega na sasa tuna Mwaka wa tatu wa Kanisa.










Akili ya Eliya Inatengeneza Maagano Kati ya MUNGU na Kanisa

1. Agano la Kuhama kituo, Kolosai 1:13, Kutoka 10:24-46
 Kuachana na nafsi ya mwili na kuingia nafsi ya roho
 Kuachana na mavazi ya zamani na kuvaa vazi jeupe
 Ninayo roho, moyo na nafsi ya MUNGU wa Eliya, Ufunuo 21:1-3
I. Sipungukiwa na lolote, Zaburi 23 
II. Ninakuwa mtakatifu maana MUNGU wa Eliya ni Mtakatifu, Walawi 19:2
III. Naendelea kumtafuta MUNGU wa Eliya, Zab.27:4
IIII. Nivema kuitwa mwana wa MUNGU wa Eliya na ndivyo nilivyo, Yohana 3:1
V. Sifa za vazi la MUNGU wa Eliya hazichunguziki, Isaya 40:28
 
2. Agano la Heri, Zaburi 1:1-3, Mathayo 5:3-11
3. Agano la Kizazi na kizazi 
4. Agano la Ukombozi
5. Agano la Amani, Isaya 9:6, Kolosai 3:15, Efeso 6:15
6. Agano la Hekima
7. Agano la Milele
8. Agano la Matengenezo
9. Agano la Kibali
10. Agano la Ulinzi wa mbele na nyuma, Zaburi 91:10
11. Agano la Uponyaji,Mathayo 9:35 ; 10:1
12. Agano la Kufunga na kufungua, Mathayo 18:18-19
13. Agano la Kutovunjwa na yeyote
14. Agano la Pasaka, Kutoka 12:12
15. Agano la Damu ya Haki,Kweli na Hukumu, Mt.26:26-27
16. Agano la Kufuta maadui wote na pote
17. Agano la Nuru
18. Agano la Marejesho
19. Agano la Upatanisho
20. Agano la Kugarikisha maadui, Mwanzo 7:17-20
21. Agano la Mamlaka
22. Agano la Uumbaji mpya
23. Agano la Kiu na njaa ya kutenda haki
24. Agano la Kumiliki na Kutawala,Mwa.1:26-28, Zab.8:6,Yos.21:43-45
25. Agano la Shika Neno, Tenda Neno, Yohana 14:21-23
26. Agano la Maongezeko
27. Agano la Kurithi, Gal.3:29
Agano la Kitabu cha Haki, Kweli na Hukumu,  2 Falme 34:14-29, 
28. Ufunuo 2:18
29. Agano la Nafsi hai, Mwanzo 2:7
30. Agano la Mti wa uzima, Mw.2:8-10,Yoh.14:6, Eze.47:12,Ufu.22:1-3
31. Agano la Usimguse Masii wa BWANA, Zaburi 105:15
32. Agano la Miaka kumi ya kanisa, Kumb.15:1-7
33. Agano la Kuomba lolote ninapewa
34. Agano la Kuanza upya
35. Agano la Kutoa zaka kamili
36. Agano la Mbingu mpya na nchi mpya
37. Agano la Hekalu
38. Agano la White Box, Mathayo 5:11-14
39. Agano la Miaka kumi ya marejesho
40. Agano la Mapenzi ya MUNGU wa Eliya yanafanikiwa
41. Agano la Kuzaa mapacha 
42. Agano la Kuteka nyara vitu vyangu, Kutoka 12:34-51
43. Agano la Kutofautishwa, Yohana 9:7, Malaki 3:16-17
44. Agano la Kubarikiwa, Mwanzo 5:11-14
45. Agano la Jiwe lisilochongwa na yeyote
46. Agano la Jiwe kuu la pembeni
47. Agano la Moto
48. Agano la Kuvuliwa aibu 
49. Agano la Majira mapya na nyakati mpya, Isa.65:13-17
50. Agano la Kutembea na miaka elfu
51. Agano la Kuangusha Adamu wa Kwanza
52. Agano la Kutembea na Adamu wa Pili
53. Agano la Kila silaha haitasima kwangu
54. Agano la Mungu wa Eliya hatatukanwa tena
55. Agano la Umoja na Mungu wa Eliya
56. Agano la Mwanzo na Mwisho
57. Agano la Lango la Neema
58. Agano la Heri tisa
59. Agano la Karama tisa 
60. Agano la Jeshi la mbinguni, Mwanzo 2:1-2
61. Agano la Mungu wa Eliya la siri
62. Agano la Madhabahu ya Eliya
63. Agano la Kuwa juu ya yote, vyote na wote
64. Agano la Kuhukumu maovu yote na waovu wote
65. Agano la Kusimamisha jua, mwezi na nyota, Yos.10:1
66. Agano la Kuleta heshima ndani ya kanisa
67. Agano la 4 11 2008
68. Agano la Vazi jeupeUfunuo 7:13-17; 3:7.
 Vazi jeupe la kujulikana na BWANA 
 Vazi jeupe la kunitoa kwenye dhiki kuu. 
 Vazi jeupe la utakaso, nimesamehewa dhambi na uovu, nimehesabiwa haki, hakuna hukumu tena juu yangu
 Vazi jeupe linaloniweka mbele za BWANA kama Eliya
 Vazi jeupe linaloniweka mbele za uwepo wa MUNGU wa Eliya
 Vazi jeupe linalo nipa kibali mbele za MUNGU wa Eliya
 Vazi jeupe linalonipa utumishi mbele za BWANA
 Vazi jeupe linalonipa kuongozwa na kuchungwa na MUNGU wa Eliya mwenyewe na Mwanakondoo anayetawala ndani ya miaka 1000
 Vazi jeupe linalonifutia kilio na maombolezo
 Vazi jeupe linalofuta vita zote
 Vazi jeupe lenye chemchemi za maji ya uzima toka kwa BWANA
 Vazi jeupe lililonipa jina jipya la kuwa nguzo katika hekalu la BWANA
69. Agano la Ahadi za MUNGU wa Eliya, Zaburi 138:2
70. Agano la Kichwa cha Israeli na Kanisa, Malaki 2:14
71. Agano la mawe manne, 1Petro 2:5-8, 1Sam.17:49, Dan.2:34-35
72. Agano la Uumbaji na kushirikishwa umbaji na MUNGU wa Eliya, Mw.2:19
73. Agano la Feet Washing, Yohana 13:1-10, Yos.1:3; 3:15-17
74. Agano la Roho Saba za MUNGU wa Eliya, Uf.5:6, Isaya 11:2, Matendo 1:8
75. Agano la Mti na matawi 50, Esta 7:7
76. Agano la Kufuta wachawi wote, Hesabu 23:13-23
77. Agano la Kusikia, kushika na Kutenda Neno, Kumb.28:1, Kut.19:5
78. Agano la Vazi la Utukufu wa MUNGU wa Eliya, Uf.21:1-13, Zek.14:21
79. Agano la shetani kumezwa, Ezekieli 28:11-18
80. Agano la Kuhama kituo, Kol.1:13, Kut. 10:24-26
81. Agano la Kibali cha Esta, Esta 5:6-7
82. Agano la Ushindi/ Shebati, Kumb. 3:14, Yos. 6:1-19
83. Agano la Kuinuliwa juu ya vilele vya vilima na milima, Mw8:4, 1Fal8:2
84. Agano la Kibanda cha Nne, Mathayo 17:1-8
85. Agano la Kuzaliwa mara ya pili, Yohana 1:12-14
86. Agano la Nuru na mchana kutobadirika, Mwanzo 8:22
87. Agano la Kushikamana na baba wa rohoni, 1Nya.11:1
88. Agano la Lango kuu la kanisa
89. Agano la MUNGU wa Eliya la kupiga maadui wote
90. Agano la Kupata raha
91. Agano la Hakuna adui asimamaye mbele yangu
92. Agano la Usiniguse
93. Agano la Majira mpya, Isaya 65:13-17
94. Agano la Milima wa rhema
95. Agano la Gharika ya silaha kizazi cha nne
96. Agano la Lango la ahadi
97. Agano la Lango la toba ya kweli
98. Agano la Damu ya gharika ya silaha
99. Agano la Damu ya ufufuo
100. Agano la Panga 3
101. Agano la Viapo 4 vya MUNGU waEliya, Yos.21:43-45
102. Agano la Ufalme usiotikisika, Danieli 2:44-45
103. Agano la Kuomba lolote na kupewa baada ya kutoa sadaka ya Nabii, 1Wafalme 3:15
104.Agano la Kulindwa ndani ya ngome ya MUNGU wa Eliya, Zaburi 9:9;27:1-14, 31:4
105. Agano la Mahali pa waovu hapapo tena
106. Agano la Kutoshindana tena
105.Agano la Pangu pote nimepewa
106. Agano la Wokovu wa kweli wa moto
107.Agano la Nguvu ya moto
108.Agano la Ngao ya moto
109. Agano la Ngome ya moto
110. Agano la Jabari ya moto
111. Agano la Boma la moto
112. Agano la Mwamba wa moto 
113. Agano la Yeyote anayenilaani amekwishauwawa
114. Agano la Ushindi

HITIMISHO

Kwa kuyatafakari yote haya yaliyoandikwa humu kwenye kitabu, utagundua kuwa Akili ya Eliya ndiyo iliyobeba unyakuo. Akili hii ya Eliya ndiyo Kizazi cha Nne cha Kanisa


The Pool of Siloam Church